Katika mpambano uliopigwa Leo kwenye dimba la taifa Dar es salaam kati ya Gor Mahia toka Kenya (Sportpesa supercup champions) dhidi ya Everton kutoka Uingereza, Everton wameibuka kidedea kwa magoli 2-1. Mpambano ulikuwa mzuri, wa kivutia, wenye mbinu nyingi za kiuchezaji na upinzani mkali. Maholi ya Everton yaliwekwa kimiani na Wayne Rooney pamoja na Kieran Dowell kwa mashuti ya mbali wakati like la Gor Mahia likifungwa kwa ufundi sana kwa kichwa na Jacques Tuyisenga kwa kuunganisha kona iliyokuwa imwchongwa. Hata hivyo kipindi cha pili ndicho kilikiwa kitamu sana kwani kila timu ilicheza kwa nguvu na ustadi ili kupata ushindi. Na hatimaye ni Everton ndio waliofanikiwa kutoka uwanjani kifua mbele. Kivutio kikubwa uwanjani hapo alikuwa ni Mchezaji machachari na maarufu aliyetokea Manchester United na kujiunga na Everton Wayne Rooney. Mashabiki wengi walionekana kuvutiwa na mwana ndinga huyo kwani wamezoea kumwona runingani pekee lakini Leo wengi walionekana kuwehuka kwa kuweza kumwo...