Yule mchezaji aliyesajiliwa na Yanga akitokea Mtibwa Sugar na ambaye aliibuka kuwa mfungaji bora wa michuano iliyomalizika hivi karibuni ya Kagame Cup, Said Bahanuz, amesema kuwa ni wakati muafaka kwake kukipiga taifa stars.
Nikilinukuu gazeti la Mwananchi Bahanuz alisema, "Nafikiri kwa sasa tuna tatizo la ufungaji timu ya taifa, naamini nitakapopewa nafasi nitaendeleza haya niliyofanya Kagame na timu kupata ushindi."Aliongeza: "Siri yangu kubwa kuibuka mfungaji bora ni kwa sababu nilimtanguliza Mungu mbele kwa kila jambo na kujituma."
"Nimezaliwa na kulelewa katika mazingira ya dini, ninamwamini zaidi mwenyezi Mungu kuliko chochote."
"Sidhani kama kweli kuna uchawi kwenye soka, ni imani potofu za watu wachache, nimejipanga kufanya vizuri zaidi na siyo kuishia hapa."
"Kila jambo nalofanya namtangulia Mungu, nafikiri ndiyo siri kubwa yangu kufanya vizuri kwenye mashindano ya Kagame." Alisema
Source: Mwananchi

Comments