Mchezaji Neymar wa Brazil jana alionesha ni kwa nini timu kubwa duniani zinamuwania kumsajili baada ya Brazil kuwa nyuma kwa goli 1 na hatimaye kushinda 3-1 kwenye mchezo wa soka uliochezwa Old Traford Jumapili. Huku Neymar akiwa mchezaji muhimu sana kwenye mechi hiyo.
Belarus waliishtua Brazil pale walipoanza kuongoza mchezo huo katika dakika ya 8 kwa goli lililofungwa kwa kichwa na Renan Bardini Bressan mbele ya umati wa watu wapao 66,000 kwenye uwanja wa wababe wa soka Manchester United.
Lakini baadaye Brazil walipambana na kufanya mashambulizi ya nguvu yaliyoongozwa na Neymar ambaye katika dakika ya 65 alipiga mpira wa adhabu uliomshinda golikipa wa Belarus Aleksandr Gutor.
Neymay akiwa anacheza katikati alimpatia krosi mchezaji wa AC Milan Pato aliyesawazisha. Brazil wakiwa wanaongoza, Neymar alimpatia pasi tena Oscar aliyefunga goli la ushindi.
Kabla ya mechi hiyo, ndani ya uwanja huo huo, Misri walilazimishwa sare ya 1-1 na New Zealand. Goli la New Zealand lilifungwa na mchezaji wa West Bromwich Chris Wood wakati lile la kusawazisha la Misri liliwekwa kimiani na Mohamed Salah.
Belarus waliishtua Brazil pale walipoanza kuongoza mchezo huo katika dakika ya 8 kwa goli lililofungwa kwa kichwa na Renan Bardini Bressan mbele ya umati wa watu wapao 66,000 kwenye uwanja wa wababe wa soka Manchester United.
Lakini baadaye Brazil walipambana na kufanya mashambulizi ya nguvu yaliyoongozwa na Neymar ambaye katika dakika ya 65 alipiga mpira wa adhabu uliomshinda golikipa wa Belarus Aleksandr Gutor.
Neymay akiwa anacheza katikati alimpatia krosi mchezaji wa AC Milan Pato aliyesawazisha. Brazil wakiwa wanaongoza, Neymar alimpatia pasi tena Oscar aliyefunga goli la ushindi.
Mpambano mkali kati ya Brazil na Belarus
Comments