Vincent Kompany amesaini mkataba wa miaka sita ndani ya timu yake ya Man City, mkataba wa kwanza mrefu kusainiwa kwenye historia ya timu hiyo.
Ni jambo lisilo la kawaida kwa timu hiyo kutoa ofa kwa wachezaji kusaini mkataba wa zaidi ya miaka mitano. Lakini mbelgiji huyo mwenye miaka 26 amekuwa mchezaji muhimu kwa Man City na alikuwa kepteni wa timu yake ilipotwaa ubingwa wa England msimu uliopita baada ya kuukosa kwa miaka 44.
"Nimekuwa hapa tangu mwanzo na nimeona mabadiliko mengi ya timu na nayajua ya ndani na nje ya timu." Alisema Kompany ambaye alijiunga na timu hiyo mwaka 2008 kutoka Hamburg SV kwa donge la dola milioni 9.25.
"Ni vizuri kujua kwamba nitaendelea kuwa Man City kwa miaka mingine sita.Najivunia kuwa timu yangu inanipenda." Aliongeza mchezaji huyo.

Vincent Kompany, mchezaji wa Man City
Comments