Timu ya Simba wapo katika hatua za mwisho kumsainisha beki wa APR, Mbuyu Twite ili kuziba pengo la Kelvin Yondani aliyetimkia Yanga.
Kwa mujibu wa Gazeti la Mwananchi, Gedfrey Nyange Kaburu alisema:-
"Ni mapema kutaja kiasi cha fedha tutakachotumia kukamilisha usajili wake, lakini wiki ijayo atatua nchi kwa lengo la kukamilisha usajili." alisema Kaburu.
Twite mwenyewe alisema anashawishika kuja kusukuma kandanda lake Simba kwa sababu viongozi wa timu hiyo wamekwishazungumza naye.
Gazeti la Mwananchi lilimnukuu mchezaji huyo akisema:-
"Ukweli ni kwamba jana kabla hatujarudi nyumbani Rwanda nilikutana na watu wa Simba tukazungumza ili nije kuichezea timu yao, niliwaambia nipo tayari ingawa hatukufikia muafaka wa moja kwa moja.Hata hivyo, hakuna shaka kwamba mambo yatakwenda vizuri na hatutashindwana kwa vile binafsi napenda kuja kucheza Tanzania," alisema Twite. Lakini hakuwa tayari kutaja dau walilokubaliana na uongozi wa Simba. Liliandika gazeti la Mwananchi. aka "Limesheheni."

Comments