Serikali imelifungia gazeti la MwanaHalisi linalotoka kila wiki kwa kile ilichodai kutoa habari za uchochezi.
Mkurugenzi wa mawasiliano katika wizara ya mawasiliano Fabian Rugaimukamu, akizungumza jana alisema kuwa kufungiwa huko kunaanza mara moja.
Kwa mijibu wa Rugaimukamu, toleo la MwanaHalisi namba 302 la Julai 11-18, namba 303 la Julai18-24 na namba 304 la Julai 25-Agosti 01 mwaka huu na mengine yaliyopita yalichapicha habari za kuitisha jamii.
Alisema pia kwamba muhariri wa gazeti hilo alishawahi kuitwa na kuonywa mara kadha lakini alikataa kutambua kwamba aliyoyaandika ndani ya gazeti lake hayakuendana na taaluma yenyewe.
“Siku zote Muhariri alijilinda kwa kunukuu kifungu namba 18 cha katiba ya Tanzania kinachotoa uhuru wa kujieleza, lakini akaepuka kunukuu kifungu namba 30, kinachoonesha mipaka ya kujieleza." Alisema.
Mkurugenzi wa mawasiliano katika wizara ya mawasiliano Fabian Rugaimukamu, akizungumza jana alisema kuwa kufungiwa huko kunaanza mara moja.
Kwa mijibu wa Rugaimukamu, toleo la MwanaHalisi namba 302 la Julai 11-18, namba 303 la Julai18-24 na namba 304 la Julai 25-Agosti 01 mwaka huu na mengine yaliyopita yalichapicha habari za kuitisha jamii.
Bwana Saed Kubenea, Mhariri Mkuu wa MwanaHalisi
“Siku zote Muhariri alijilinda kwa kunukuu kifungu namba 18 cha katiba ya Tanzania kinachotoa uhuru wa kujieleza, lakini akaepuka kunukuu kifungu namba 30, kinachoonesha mipaka ya kujieleza." Alisema.
Muhariri mkuu wa MwanaHalisi Saed Kubenea
alisema alisikitishwa na serikali kwa kitendo cha kulifungia gazeti kwa sababu hakupewa nafasi ya kusikilizwa.
“Kama MwanaHalisi limetuhumiwa kwa kuchapisha mambo ya uchochezi, sasa kati ya serikali na mahakama, ni chombo kipi kina mamlaka sahihi ya kushughulikia jambo hili?” Aliuliza.
Source: IPPMEDIA
Source: IPPMEDIA
Comments