Mwanamuziki Snoop Dogg wa Marekani mwezi uliopita alizuiliwa kwenda nchini Norway kwa miaka miwili kutokana na kile kilichodaiwa kutaka kuingia nchini humo akiwa na Marijuana ama maarufu kama bangi.
Dogg alitakiwa kufanya onesho huko Arendal, Norway tarehe 28 Julai wakati alipozuiliwa na maafisa wa mpakani baada ya mbwa wa kunusa madawa kumgundua. Alikutwa na gramu 8 za bangi kwenye begi lake pamoja na kiasi kikubwa cha fedha kinyume na taratibu. Baada ya kukubali kosa alitozwa faini ya dola 8,600.
Mwanasheria wake alisema kuwa Dogg hana haja ya kukata rufaa yoyote.
Mwanamuziki huyo raper ambaye anatarajia kutoa albamu ya rege mwishoni mwa mwaka huu itakayoitwa Snoop Lion, pia aliwahi kutiwa nguvuni huko Texas mwezi Januari wakati mbwa wa polisi walipomkuta na bangi kwenye begi chafuchafu ndani ya basi lake.

Snoop Dogg

Comments