Ugonjwa wa ebola ambao unaua watu kwa haraka sana ulianza mwanzoni mwa mwezi Julai huko mashariki wa Uganda na tayari umeua watu 14. Shirika la afya duniani lilisema siku ya Jumamosi.
Ugonjwa huo ulianzia mashariki mwa wilaya ya Kibaale, kama kilometa 200 kutoka mashariki mwa mji mkuu wa Uganda, Kampala, na kama kilimeta 50 toka mpakani na Nchi ya Kidemokrasia ya Kongo.
"Tumethibitisha watu 20 kuambukizwa virusi vya ebola ambapo miongonimwao 14 wamekwishafariki" Alisema Joaqim Sewaka, mwakilishi wa shirika la afya duniani.
Alisema pia kuwa timu za wizara ya afya Uganda na kituo cha kudhibiti magonjwa cha Marekani, Centre for Disease Control (CDC), vimewasili eneo lililoathirika.
Ugonjwa huo ulioitwa kwa jina la mto mmoja huko Kongo, uliua watu 37 mashariki mwa Uganda mwaka 2007 na watu 170 kaskazini mwa nchi hiyo mwaka 2000.

Mgonjwa wa ebola akiwa anahudumiwa hospitalini
Comments