Mwanamuziki wa Uganda Joseph Mayanja ama maarufu kama Jose Chameleon, siku ya Alhamisi alileta vurugu kwenye ubalozi wa Tanzania mjini Kampala pale alipoweka kambi kwenye lango kuu la ubalozi huo akidai arudishiwe paspoti yake.
Alilala kwenye mkeka tangu saa 9 usiku na kjifunika kwa blanket na shuka hadi alfajiri.
Wanachama wa Leone Island Group waliungana naye na kunyoosha mabango wakimtaka balozi awasaidie kurejesha paspoti zao, Miongoni mwao walikuwemo Dj wake Sulaiman Kaliisa na Denis Kibalama.
Polisi waliingilia kati na kulizingira eneo hilo kisha kumhoji Jamaa huyo kwa muda na kuwaomba waondoke eneo hilo lakini walikataa.
IGP Lt. Kale Kayihura aliingilia kati na kuwakusanya Jose Chameleon na kundi lake kwenye kituo cha community police post.
Kundi la waendesha bodaboda walimsindikiza huku wakipiga honi na kuliimba jina lake njia nzima wakielekea kituoni huko.
IGP aliwasiliana na watu huku Tanzania ili wafuatilie jambo lake kwa mfanyabishara Eric Shigongo juu ya kupata paspoti yake.
Shigongo alizizuia paspoti hizo baada ya onesho la Chameleo lililopaswa kufanyika tarehe 7 Julai baada ya kutoa advance ya dola za Marekani 3500 lakini hakuonekana, Jambo ambalo Chameleon amelikana. Na ndipo Chameleon na kundi lake walipata paspoti za muda na kuondoka.
Lakini wiki mbili baadaye poli wa Kampala walimkamata jamaa mmoja aitwaye George Mugabe baada ya Chameleo kudai kwamba alijifanya meneja wake na kupokea pesa kwa niaba yake. Lakini baadaye aliachiwa.
Kayihura aliahidi kulifuatilia suala lake na kumuomba aachane na maandamano yake.

Jose Chameleon akiwa kwenye maandamano na kundi lake
akiwa amebeba bango lisemalo "Nahitaji kurudishiwa paspoti yangu"

Comments