Meneja wa Arsenal, Arsen Wenger amesema leo kwamba hajapata ofa toka kwa timu yoyote ya kutaka kumnunua Van Persie ambaye anawaniwa na Manchster City, Manchester United na Juventus.
Mustakabali wa mchezaji huyo umekuwa ukizungumziwa sana hasa baada ya yeye mwenyewe kusema kuwa hayuko tayari kutia saini kuichezea timu hiyo ya washika bunduki wa London mara mkataba wake utakapoisha.
Akizungumza huko Uchina, Wenger alisema, "kwa wakati huu suala la Van Persie halijatusumbua sana. Hatujapata ofa yoyote, kwa hiyo yeye ni mchezaji wetu. Kwa hiyo sidhani kama tunahitaji kuzungumzia jambo hili tena."
Inasemekana kuwa Arsenal wanahitaji kiasi cha pauni milioni 20 kwa ajili ya kumuuza msukuma kandanda huyo.
Sakata la Van Persie limekuja baada ya Wenger kuwapoteza wachezaji wake muhimu sana msimu uliopita ambao ni Samir Nasri aliyeenda Man City na Sesc Fabregas aliyeenda kuupiga mpira Barcelona.
Meneja wa Man City, Roberto Mancini alipoulizwa juu ya madai ya Wenger alisema, " Nadhani kama Wenger alisema hivyo basi ni kweli.Hilo ni jambo gumu kwa sababu Van Persie ni mchezaji mashuhuri duniani na ni mfungaji mzuri sana kwa hiyo ni ngumu sana kumnunua." Alipoulizwa endapo wao Man City wametoa dau la kumnunua alisema, "Hapana, sidhani."

Robin Van Persie ambaye mstakabali wake umejaa utata mpaka sasa

Comments