Timu ya Yanga ambayo wiki iliyopita walichukua kwa mara nyingine kombe la Kagame baada ya kuichapa bila huruma timu ya Azam 2-0, imeendelea kujiimarisha kwa kumsainisha mchezaji maarufu Didier Kavumbagu kutoka Burundi.
Gazeti la Championi liliandika kwamba baada ya kumtilisha saini msukuma kandanda huyo wa Burundi, imetangaza kufunga usajili na sasa kuelekeza nguvu zake kwenye maandalizi ya ligi msimu ujao.
Mchezaji huyo anatarajia kurudi nchini keshokutwa ili ajiunge na wenzake kule Jangwani yalipo makao makuu ya wababe hao wa Afrika Mashariki na Kati.
Kavumbagu ndiyo yule aliyeifungia Atletico ya Burundi magoli 2 ambayo yaliizamisha Yanga kwenye mchezo wao wa ufunguzi wa kombe la Kagame.
Nikilinukuu gazeti la Championi ambalo nalo lilimnukuu Seif Ahmed anayehusika na mambo ya usajili aliyesema:-
“Kweli tumemalizana naye na ameishasaini kuichezea Yanga, yalikuwa ni maoni ya pamoja kati ya kocha na kamati yetu maalum. Kuanzia hapa nafikiri tutakuwa tumefunga usajili,”

Wasukuma kandanda wa Jangwani, Yanga Africans
wakiwa na jezi ya Njano ambayo ni maarufu sana
Hapa wakiwa na jezi ya kijani ambayo
nayo ni maarufu sana Jangwani
Na huyu ndiyo mwenyekiti wa Yanga, Bwana Yusuf Manji
Na huyu ndo kocha mkuu wa Yanga
Tom Saintfiet
Comments