Zaidi ya kilogramu 900 za bangi yenye thamani ya shilingi milioni 9 zilikamatwa jana Alhamisi na maofisa wa mamlaka ya mapato ya Kenya mpakani mwa Kenya na Tanzania.
Bangi hiyo iliyokuwa ndani ya magunia 31 ilikuwa ikisafirishwa kwa lori ambalo baada tu ya kukatiza mpaka kuingia Kenya maofisa walilitilia mashaka.
"Maofisa walikuwa wakifanya ukaguzi wao wa kawaida tu wakati walipoikuta bangi imefichwa kwenye lori hilo." Alisema msemaji wa Mamlaka ya Mapato Kenya bwana Kennedy Onyonyi.
Dereva wa lori hilo alitoroka mara moja wakati polisi wakilikagua lori lake na wameamua kufanya doria ya kumsaka maeneo ya Namanga, mpakani mwa Kenya na Tanzania.
Kufuatia tukio hilo, polisi wa Kenya wamemua kuweka ulinzi mkali ili kuzuia uingizaji wa bangi nchini mwao kutokea Tanzania.
Haya ndiyo magunia ya bangi yaliyokuwa yanaingizwKenya
kutokea Tanzania

Comments