Manchester City Dhidi Ya Liverpool
Hii ilikuwa ni Man City dhidi ya Liverpool. Ilikuwa ni moja ya mechi nzuri na kali sana tangu kuanza kwa English Premier League.
Liverpool walionekana kujipanga vizuri zaidi na kuwapa shida sana walinzi pamoja na viungo wa Man City.
Kama siyo makosa ya walinzi wa Liverpool ambao kwa namna moja au nyingine tunaweza kusema ndiyo waliochangia Man City kusawazisha magoli basi stori leo zingekuwa nyingine kabisa.
Magoli ya Man City yalifungwa na Yahya Toure na Carlos Tevez na yale ya Liverpool yalifungwa na Martin Skrtel pamoja na Suarez
Juu: Tevez alimpiga chenga kipa wa
Liverpool na kusawazisha goli la pili
kwa Man City baada ya mlinzi wa
Liverpool Martin Skrtel kufanya
makosa ya kurudisha mpira kwa
goli kipa bila kuangalia kama kuna adui ama la.
Juu: Hapa Tevez akishangilia baada ya
kufunga goli la pili kwa timu yake
Juu: Man City wakipongezana baada
ya kusawazisha goli la kwanza
kupitia Yahya Toure.
Juu: Huyu ni kijana mdogo sana
Raheem Sterling, Winga wa kushoto,
mwenye umri wa miaka 17 tu.
Alionesha kipaji cha hali ya juu na
kusumbua sana walinzi wa Man City.
Arsenal Dhidi Ya Stoke City
Arsenal walishindwa kwa mara ya pili mfululizo kuwaridhishwa mashabi wao baada ya kutoka sare tena kwenye mchezo wao huo wa jana.
Hawa ni mashabiki wa Stoke City
wakiwa na Mask za Arsene Wenger
kocha wa Arsenal
Hapa kulikuwa na mpambano
mkali sana kati ya Peter Crouch
wa Stoke na walinzi wa Arsenal
Manchester United Dhidi ya Fulham
Man United walinda magoli 3-2 dhidi ya Fulham. Ikumbukwe kuwa mechi yao ya kwanza walifungwa na Everton 1-0.
Huyu hapa juu ni Usain Bolt,
mfukuza upepo maarufu sana,
raia wa Jamaica ambaye ametokea
kuwa mshabiki mkubwa wa
Manchester United. Hapa alikuwa katikati ya
uwanja kabla ya kuanza kwa mechi
ya Man United dhidi ya Fulham.
Wayne Rooney akipelekwa nje baada
ya kujeruhiwa vibaya sana kwenye paja lake.
Inasemekana atakaa nje ya dimba kwa
wiki nne mfululizo akiuguza jeraha.
Usain Bolt na ushabika wake kwa Man United.
Wayne Rooney akichati na Welbeck kabla hawajaingia uwanjani
Robin Van Persie akifunga goli la kusawazisha
kwa Man United kwa ufundi wa hali ya
juu kama ilivyo kawaida yake.
Na hili ndilo goli lake la kwanza tangu
ajiunge na Man United.
Shinji Kagawa akishangilia baada ya
kufunga goli la pili kwa Man United
Rafael Da Silva akishangilia baada ya
kufunga goli la tatu kwa Man United
Juu na chini, hapa ndiyo wakati
Wayne Rooney anaumia
Chelsea Dhidi Ya Newcastle
Chelsea waliwafunga Newcastle magoli 2-0
Juu: Eden Hazard
Torres akishangilia goli
Comments