Hatimaye Dimitr Berbatov anahama Man United na kuelekea Fulham kwa donge la dola milioni 5.
"Berbatov anamalizia vipimo vyake na kama mambo yataenda vema atakuwa moja ya wachezaji wetu. Kulikuwa na timu nyingi zilikuwa zinamuhitaji lakini sisi tulikuwa na uwezo wa kumpata. Alikuwa kwenye list yangu wakati wote. Nilijaribu kumfuatilia miezi kadhaa iliyopita lakini sikufanikiwa hivyo nilirudi tena na sasa ulikuwa ni wakati muafaka kwa yeye kufanya maamuzi." Alisema Martin Jol kupitia Fulham FC.com.
Berbatov alienda Man United akitokea Tottenham Hotspur mwaka 2008 kwa rekodi ya uhamisho wa dola milioni 30, kitu ambacho kinaonekana hakijaendana na uwezo wake wa kazi awapo uwanjani.
Lakini kama isingekuwa uwezo wake wa ajabu wa kipindi cha kwanza mwaka 2010-2011, Man United wasingeweka rekodi ya kuchukua kombe la ligi mara 19 msimu huo.
Berbatov alikuwa kwenye msimu wa mwisho wa mkataba wake, na kwake yeye mwenye miaka 31 kupata mkataba wa dola milioni 5 siyo biashara mbaya. Hasa ikizingatiwa kwamba thamani yake kama ilielekea kushuka na timu zilizomuhitaji zililijua hilo.
Man United wakiwa na washambuliaji kama Wayne Rooney, Robin Van Persie, Danny Welbeck na Javier Hernandez, Berbatov asingekuwa kwenye mpango wa Ferguson kama ilivyokuwa msimu uliopita.

Comments