Skip to main content

"Hatutamwongezea Mshahara Walcott," Asema Wenger

Arsene Wenger alisisitiza jana kwamba bado anajaribu kumshawishi Theo Walcott kusaini mkataba mwingine na Arsenal, lakini akamwambia winga huyo kwamba sheria za mishahara hazitapindishwa kwa sababu yake.


 Theo Walcott

Walcott ameruhusiwa kuendelea na mkataba wa mwaka mmoja wa mwisho, hatari ambayo Arsenal waliikwepa kipindi cha nyuma walipomuuza Robin Van Persie hivi karibuni na Samir Nasri mwaka jana.

Walcott atakuwa huru kuondoka msimu ujao wa joto (summer) endapo mkataba wake utafika kikomo, lakini Wenger ana uhakika zaidi kwamba atabakia kuliko alivyowafikiria Van Persie na Nasri.
"Theo ana miaka 23 tu, ni mwingereza, anaishi mwendo wa dakika 10 tu toka hapa. Hivyo natumaini tutafikia makubaliano." Alisema Wenger.

Arsenal hawana mpango wa kulipa wachezaji viwango vya juu sana na Wenger aliweka wazi kabisa kwamba hivyo ndivyo ilivyo. "Kila maamuzi yana mpangilio wake na hicho ndiyo kiwango chetu cha mshahara na tunakiheshimu. Kama hatutafanya hivyo hatutafika popote. Hakika ni tofauti kwa mchezaji mwenye miaka 29 na yule wa 23. " Alisema Wenger.

Wenger akiwa kazini

Wenger pia alimtetea Walcott kwamba yeye siyo mpenda pesa. "Hajatawaliwa na pesa. Zipo tofauti kidogo kwenye makubaliano ambazo lazima zitokee.

Wakati mazungumzo bado yanaendelea msimu huu, Walcott atabakia Arsenal, na Wenger ana wasiwasi kidogo juu yake. "Sijui nini kitatokea Januari," alisema Wenger. "Nina wasiwasi zaidi kuhusu Jumatatu (wakati Arsenal watakutana na Liverpool huko Anfield). Theo yupo kwenye mazoezi na anatarajiwa kufanya vizuri, na kinachotokea mwisho wa msimu kinatokea mwisho wa msimu."

Adabu ya Walcott ilielezwa na Wenger kuwa ni "Fantastic." Alipoulizwa ana uhakika gani juu ya commitment ya Walcott kwa Arsenal, Wenger alijibu, "Bado hatujapata mashine itakayopima nguvu au kiwango cha mapenzi ya mtu kwa timu, wote tungeinunua mashine hiyo."

Wapenzi wengi wa Arsenal wanataka timu itumie pesa lakini Wenger anasema hawatafanya hivyo kwa ajili ya kuikoa timu. "Kutumia pesa sio ubora. Kununua wachezaji wazuri ndiyo ubora, wachezaji wazuri zaidi ya uliokuwa nao ni bora. Tutafanya matumizi ya pesa tutakapopata wachezaji sahihi." Alisema Wenger.

Comments

Popular posts from this blog

MAKUNDI CHAMPIONS LEAGUE NA SHIRIKISHO AFRIKA

Yanga Sc kundi A Klabu Bingwa Afrika na Simba Sc kundi A Shirikisho Afrika. Hapo chini ndio mpangilio wa makundi na timu zake. Je, nani kati ya timu zetu za bongo atatoboa kwenda robo fainali? Weka maoni yako kwenye komenti tafadhali.

Hawa Ndiyo Real Madrid Waliowafunga Man City Champions League Jana Usiku

Man City wakiwa wanaongo za kwa 2-1 dhidi ya Real Madrid huku zikiwa zimebaki dakika si zaidi  ya tatu walionekana kama ingekuwa ni timu ya tatu ya Uingereza kuifunga Madrid kwenye uwanja wa Bernabeu. Lakini vijana hao wa Mancini badala ya kuinza kampeni yao kwa ushindi walijikuta wakiachwa nyuma na kuwaangalia Madrid wakiibuka na ushindi baada ya Karim Benzema kusawazisha na kisha Cristiano Ronaldo kufunga goli la tatu na la ushindi, goli lililomfanya bosi wao Jose Mourinho kuslide uwanjani akishangilia goli hilo na Ronaldo. This was the real happiness now from Ronaldo BBC football pundit Robbie Savage alikuwa uwanjani huku Bernabeu. (quoting from BBC SPORTS) "Maicon was not at the races at all in the first half at right-back. He was a passenger and it was like City were playing with 10 men. Cristiano Ronaldo kept coming inside him. "In the second-half, Vincent Kompany looked at what was happening and came across to that wing more. Ronaldo did not...