Usain Bolt amejizolea sifa kubwa
sana duniani baada ya kuonesha
umwamba wake wa mbio za mita
100 na 200 kwenye michezo ya
Olympic iliyofanyika mwezi uliopita
huko London Uingereza.
Mara zote alikuwa anatamba kwamba
atashinda kabla ya mbio kufanyika
na wakati wa mbio ndicho alichofanya
na kusababisha watu wengi wa
mataifa mbalimbali kuvutiwa
naye na kumpenda sana.
Ilifikia hata watu wa mataifa mengine
walimshangilia kwa nguvu zote
Imegundulika kwamba Usain Bolt
ni mshabiki mkubwa sana wa
Man United na anapokuwa
England hujaribu kuhudhuria
mechi zote za Mashetani hao wekundu.
Kuna wakati alisikika akisema
kwamba anamwomba Sir Alex Ferguson
amsajili kwenye kikosi chake
kwani pamoja na kuwa na wachezaji
wenye vipaji pia timu inahitaji
wachezaji wenye mbio kama yeye.
Comments