Tunaweza kuwaita ni wachezaji wa dunia kwani hata watoto wadogo wanawafahamu hawa zaidi kuliko wachezaji wengine wowote. Hiyo inatokana na ukweli usiofichika kwamba ni wachezaji muhimu sana kwenye timu zao na wanafanya yale ambayo timu na makocha wao wanatarajia na hivyo kuwafanya wabakie kwenye nafasi za juu ulimwenguni na kumzo kubwa.
Messi na Ronaldo wakisalimiana
Wakati msimu wa ligi ya Hispania maarufu kama "Primera La Liga" ndiyo umeanza hivi karibuni, yameibuka maswali mengi sana miongoni mwa mashabiki wa Lionel Messi anayechezea Barcelona na wale wa Christiano Ronaldo anayechezea Real Madrid kwamba "nani atakuwa zaidi ya mwenzake msimu huu?."
Messi akifanya vitu vyake uwanjani
Ronaldo huwa anaifunga Barcelona pale wanapokutana na Messi vivyo hivyo. Jambo ambalo linafanya swali la nani zaidi kuwa gumu sana kujibika kutokana na ukweli kwamba wote wawili ni wakali sana na kama mmoja anmzidi mwenzake basi ni kidogo sana.
Yule mkimbiaji maarufu wa Jamaika, Usain Bolt aliwahi kusikika akisema kwamba siyo kweli kwamba Messi ni zaidi ya Ronaldo bali alidai kwamba Ronaldo ndiyo zaidi ya Messi.
Sijajua kama aliyasema hayo kwa sababu yeye ni mpenzi mkubwa wa Man United alikokuwa anachezea Ronaldo ama la.
Ronaldo akishangilia goli baada ya kuwafunga Barcelona
Jambo la kufanya kwa mashabiki wa soka ni kusubiri na kujionea wakati mechi mbalimbali zitakapokuwa zikichezwa na timu hizo mbili zinazoongozwa na wachezaji hao wawili wenye umaarufu mkubwa duniani.
Wewe unasemaje? unalo jibu la nani zaidi kati ya Ronaldo na Messi?
Comments