Valencia akiwa kwenye moja ya harakati zake za kuchonga krosi
Alijiunga na Manchester United mwaka 2009 kwa donge la dola milioni 17. Naye ni raia wa Ecuador. Ilikuwa ni wakati Christiano Ronaldo anahamia Real Madrid na kuacha pengo kubwa sana kwa Man United. Pengo ambalo hakuna aliyewahi kuwaza kwamba lingezibika.
Lakini mara alipoanza kuichezea Man United alianza kuonesha kwamba anaweza kwani mbio pamoja na krosi zake kuelekea upande pinzani vilikuwa ni hatari tupu.
Alianza vizuri sana lakini akakumbwa na balaa la kuumia kiasi kwamba alikaa nje ya dimba kwa muda na kufanya watu washindwe kushuhudia uwezo wake vizuri.
Msimu uliopita ndipo watu walipoona umuhimu wake na kipaji chake na kugundua kwamba ni winga wa kiwango cha juu sana. Akiwa na uwezo wa kukimbia na mpira kwenye wing ya kulia na kuachia mashuti yake ya krosi kama risasi zikiwa zinawalenga Wayne Rooney pamoja na Javier Hernandez.
Winga huyo ambaye watu hudhani ni old fashion, hapendi sana kupiga chenga badala yake ni kukimbia na kutoa krosi, alifunga magoli 6 na kusababisha 13, huku ni David Silva pekee akiwa juu yake kwa kusababisha magoli 15 kwenye mechi nyingi.
Msimu ambao alifanya juhudi sana bila kuchoka na mashabiki wa Man United wakamzawadia "Mchezaji bora wa mwaka" na zawadi ya goli la msimu kwa goli alilofunga walipocheza dhidi ya Blackburn Rovers.
Udhaifu pekee ambao mashabiki wa Man United wanauona kwake ni kule kushindwa kwake kutumia mguu wa kushoto wakati wa mchezo. Japo alijaribu kupiga krosi kwa mguu wa kushoto pale walipopambana na Fulham.
Ni mchezaji ambaye kwa kweli anastahili kuwa hapo alipo leo. Valencia, mwenye miaka 27 sasa, ana uwezo bado wa kukuza soka lake na kuwa moja ya wachezaji wa kukumbukwa duniani. Hakuna maswali mengi sana juu ya hilo kwani sasa anavaa namba ya jezi iliyovaliwa na wachezi maarufu sana duniani.
Wewe unasemaje kuhusu Valencia?
Comments