Anaitwa Theo Walcot. Inasemekana Manchester City wanampango wa kutangaza dau la kumnunua mchezaji huyo baada ya kugundua kwamba anaweza asitie saini yake tena kuichezea Arsenal.
Inasemekana Roberto Mancini anavutiwa sana na fowadi huyo wa Arsenal kwa muda mrefu sana kiasi kwamba huenda akatangaza dau ingawaje na Liverpool nao inaonekana wana lengo kama hilo.
Mshauri wake alianzisha mazungumzo na Arsenal Ijumaa iliyopita ya kuhusu mkataba mwingine wa miaka mitano wa dola 75,000 kwa wiki, walakini wawakilishi wake inasemekana wanataka kuikataa ofa hiyo.
Katika mazungumzo mengine ya Jamanne, Arsene Wenger akiwa anatamani kumbakiza winga wake huyo, yeye pamoja na uongozi wa club wamesema kwamba wanatarajia kumuuza mchezaji huyo kabla ya kufungwa kwa pazia la usajili Ijumaa kama hawatasikia chochote toka kwake kama anataraji kuendelea na Arsenal.
Comments