Eto'o alitumikia kifungo cha kucheza soka la kimataifa kwa miezi nane na alikataa kushiki timu yake ya taifa, "Indomitable Lions" kwenye mechi yao dhidi ya Cape Verde, lakini sasa anatarajia kurudi kundini.
Samuel Eto'o
"Kwa ombi la nchi yangu, naamua kurudi Indomitable Lions," Alisema.
"Natiwa moyo na shauku yangu ya kuitumikia nchi yangu kwa imani ile ile ya miaka 15 iliyopita.
Meneja Song Bahang na kocha Jean Paul Akon wote walikuwepo wakati wa mikutano ya makubaliano hayo ya kumwomba Eto'o kurudi dimbani, na Eto'o ambaye ameshatingisha nyavu mara 53 katika mechi 109 za taifa alizocheza anaamini kwamba ataweza kufanya kazi pamoja timu yake ya makocha ili kuleta mafanikio zaidi kwa taifa lake.
"Nilikutana na mamlaka ya taifa hivi karibuni ili kujadili hali ya hivi karibuni ya soka la Cameroon, na hususan timu ya taifa." Alisema.
"Nashawishika kwamba kwa pamoja, tukiweka mbali matakwa yetu binafsi na kuzingatia yale ya kitaifa, tunaweza, na kwa uwezo wa Mungu wa kuifanya Camerron ing'ae."
Comments