Skip to main content

Roberto Di Matteo na Mechi ya Leo Dhidi ya Arsenal

Pamoja na kwamba mwisho wa wiki hii unaonekana ni mgumu sana kwa kocha wa Chelsea Roberto Di Matteo, lakini yeye mwenyewe anasisitiza kwamba hatishwi wala kuogopeshwa jinsi timu yake inavyoonekana kwa nje, yaani mitazamo ya watu. 

Roberto Di Matteo

Kepteni wa Chelsea John Terry amesimamishwa na chama cha soka huko Uingereza kutocheza michezo minne kutokana na katabia kake alikokaonesha ka ubaguzi wa rangi dhidi ya Anto Ferdinand msimu uliopita.  

 Anton Ferdinand na John Terry

Anton Ferdinand

Ingawaje Di Matteo, hataruhusu hukumu maneno yoyote toka nje ya kuhusu Chelsea ili isije wasumbua wachezaji wake na club kwa ujumla. 

"Tunajiamini ," alisema Di Matteo kuhusu mechi yao na Arsenal mchana wa leo. "hivyo hatujali sana kitu gani watu huko nje hunena juu yetu. Ni lazima tujiangalie nguvu yetu juu ya mchezo na huo ndiyo mwenendo wetu."  

"Hivyo ndivyo nionavyo na nihisivyo. Siwezi kuwaza eti watu wengine wana maoni gani. Tunachoweza kufanya ni kuwaza ni namna gani tunacheza na tunavyojiheshimu na kujitunza. Lazima tujiweke kwenye hali nzuri. Na hata mwisho wa siku tunajua kwa hakika wapenzi wa timu pinzani hawatatupenda."

"Hayo ndiyo maneno yangu kwa ujula. Hivyo hatutapoteza nguvu nyingi kuwa na wasi wasi juu  ya nini wanawaza. Ni lazima tujifikirie wenyewe, tujaribu na kushinda mechi kwa timu yetu."  


Terry atakuwepo kwenye mechi ya leo, pamoja na kukosa siku kadhaa za mazoezi ili ahudhurie kesi yake huko Wembley. 

Di Matteo alisema kwamba kila kitu kitaendelea kama kawaida na kwamba atachagua timu yake kwa mujibu wa Emirates pekee. 

"Uchgauzi wangu mimi ni wa kawaida tu." Alisema Di Matteo. "Ninavyoweza kuona Terry yupo fit. kutakuwa na taratibu za kawaida tu. Itakuwa ni kazi yangu kuchagua timu itakayoipiga Arsenal." 

Terry ana uwezo wa kucheza vizuri tu bila kujali mambo ambayo inaonekana yatawachanganya wengine, na Di Matteo anaona hakuna chochote cha kupoteza leo. 

Wakati bosi wa Chelsea alieleweka kuchukua tahadhari kuzungumzia ishu za hivi karibuni, alimsifu kwa hasaka Terry na tabia yake kwa upande wa kazi awapo uwanjani. "Niwezayo kusema ni kazi yake awapo kwenye timu." Alisema Di Matteo.

"Siku zote yeye ni wa kwamba kuwasili. Ana jitihada sana na amekuwa ni mtumishi mzuri sana wa timu yake. 

Chelsea walianza Premier League vizuri na wapo kileleni, lakini Arsenal watakuwa ni wapinzani wao hatari sana kwa msimu huu.  

"Utakuwa ni mtihani mgumu, alikubali Di Matteo. "Arsenal siku zote ni mtihani mgumu, ni changamoto kubwa kwetu. Lakini na kwao pia itakuwa ni changamoto kubwa, kwani sisi ni timu ngumu na nzuri pia.  

Ingawaje Arsenal walimuuza Robin van Persie na Alex Song, Di Matteo alisema alitabiri kwamba wangekuwa ni tishio kwao tangu mwanzo. 

"Nilisema mwanzoni mwa msimu kwamba Arsenal wataleta changamoto kwenye ligi," alisema meneja huyo. "Sina uhakika kama kuna aliyeniamini, lakini hivyo ndivyo nilivyooona mimi, na sijabadili mawazo yangu."  

"Sidhani kama wana namna nyingine tofauti ya kucheza. Wanacheza kwa kumiliki sana mpira na kuutafuta wanapoupoteza, lakini  Lukas Podolski na Gervinho wamekuwa wakifunga magoli, na Santi Cazorla. Wanao wachezaji ambao ni tishio na wenye uwezo wa kubadilisha nafasi." Alisema Di Matteo.

Kama wewe ni mshabiki wa Arsenal au Chelsea, unasemaje kuhusu mechi ya leo?

Comments

Popular posts from this blog

MAKUNDI CHAMPIONS LEAGUE NA SHIRIKISHO AFRIKA

Yanga Sc kundi A Klabu Bingwa Afrika na Simba Sc kundi A Shirikisho Afrika. Hapo chini ndio mpangilio wa makundi na timu zake. Je, nani kati ya timu zetu za bongo atatoboa kwenda robo fainali? Weka maoni yako kwenye komenti tafadhali.

Hawa Ndiyo Real Madrid Waliowafunga Man City Champions League Jana Usiku

Man City wakiwa wanaongo za kwa 2-1 dhidi ya Real Madrid huku zikiwa zimebaki dakika si zaidi  ya tatu walionekana kama ingekuwa ni timu ya tatu ya Uingereza kuifunga Madrid kwenye uwanja wa Bernabeu. Lakini vijana hao wa Mancini badala ya kuinza kampeni yao kwa ushindi walijikuta wakiachwa nyuma na kuwaangalia Madrid wakiibuka na ushindi baada ya Karim Benzema kusawazisha na kisha Cristiano Ronaldo kufunga goli la tatu na la ushindi, goli lililomfanya bosi wao Jose Mourinho kuslide uwanjani akishangilia goli hilo na Ronaldo. This was the real happiness now from Ronaldo BBC football pundit Robbie Savage alikuwa uwanjani huku Bernabeu. (quoting from BBC SPORTS) "Maicon was not at the races at all in the first half at right-back. He was a passenger and it was like City were playing with 10 men. Cristiano Ronaldo kept coming inside him. "In the second-half, Vincent Kompany looked at what was happening and came across to that wing more. Ronaldo did not...