Skip to main content

Spurs Yawachapa Kipigo Red Devils

Clint Dempsey jana aliwathibitishia ushindi Tottenham kwa mara ya kwanza wakiwa Old Trafford tangu  December 1989 baada ya kuwapa kipigo mashetani hao wekundu (Man United) na kuwafanya kupoteza mchezo wa pili tangu kuanza kwa ligi hiyo ya Uingereza. 

Huyu ndiye Clint Dempsey akishangilia goli

Wakiwa wanaongoza 2-0 hadi half-time, Spurs walikianza kipindi cha pili kwa kuruhusu goli toka kwa Man United lililofungwa na Luis Nani aliyepokea krosi toka kwa Wayne Rooney ambao waliingia kipindi cha pili kama simba aliyejeruhiwa, lakini muda mfupi tu baada ya kuruhusu goli hilo walipiga tena goli la tatu na kuwafanya vijana wa Man United wachanganyikiwe. Lakini Man United walijitahidi kucheza bila kuonesha kama wamechanganyikiwa na kuelekeza mashambulizi makali langoni mwa Spurs huku wakicheza kandanda safi lililowafanya Spurs kupaki gari kuanzia katikati ya uwanja hadi ndani ya eneo lao la 18, huku Rafael, Wayne Rooney, Evra na hata Rio Ferdinand wakipeleka krosi za kila mara langoni mwa wapinzani wao wakijaribi kutafuta kusawazisha na hata kupata goli la ushindi. Lakini alikuwa ni Shinji Kagawa aliyewapatia Man United goli la pili na la mwisho na kuufanya mchezo kwisha kwa Spurs kuibuka kwa ushindi wa 3-2.

Spurs wakiwa bado hawajapoteza mchezo tangu kufunguliwa kwa ligi hiyo, wanajipatia umaarufu na kujiamini sana chini ya kocha wao Andre Villas-Boas, aliyekuwa kocha wa zamani wa Porto. 

Kuumia kwa Nemanja Vidic kulileta pengo kubwa sana kwa upande wa Man United na kusababisha katikati kuwe na kichochoro ambacho kiliwapatia Spurs urahisi wa kufunga magoli  yao. Pamoja na wachezaji wakongwe Ryan Giggs na Paul Scholes, bado kullikuwa na udhaifu mkubwa kwani Spurs walionekana wenye mbio na nguvu wakiwa na maumbo makubwa zaidi ya Man United. 

Giggs na  Scholes wanashindwa siku hizi kuonesha ule umaarufu wao wa kutawala kiungo na ile tabia ya Giggs kupiga krosi zinazowarahisishia wafungaji kupata magoli mazuri. Kwani walionekana kuzidiwa sana na wachezaji wenye kasi na nguvu nyika Gareth Bale na Moussa Dembele, na kufanya kuonekana kama vile chaguo la Ferguson ni ajali iliyokuwa inasubiriwa kutokea. 

Pamoja na kwamba hakukuwa na wa kumlaumu kati yao kwa goli la Vertonghen kwenye dakika ya 2 tu ya mchezo, lakini ilioneka wazi aliachiwa nafasi ya wazi ya kukimbia kuanzia katikati ya dimba kabla ya kufunga goli. 

Vertonghen, aliyetokea Ajax, aliwapita Nani na Rio Ferdinand wakati alipokimbia kwa mita 35 na shuti lake kumgonga beki wa Man United John Evans kabla halitinga wavuni.

Chelsea wameendelea kubakia kileleni baada ya Juan Mata kuifanya iibuke kwa ushindi wa 2-1 ugenini dhidi ya Arsenal. Wapo pointi 3 mbele ya Everon ambao nao waliendelea na ushindi wa 3-1 dhidi ya Southampton. 

Mabingwa watetezi wa Premier League Manchester City wakitokea nyuma walishinda 2-1 dhidi  ya Fulham, wakimuingiza Edin Dzeko aliyewapatia goli la ushindi dakika 3 kabla ya mtanange kuisha.

 

Comments

What an enjoyable time to look through to this post thanks for the sharing and keep it up.
RKAY said…
Thank you very much. It means a lot to me. I sure will keep it up. Join in me almost everyday.

Popular posts from this blog

MAKUNDI CHAMPIONS LEAGUE NA SHIRIKISHO AFRIKA

Yanga Sc kundi A Klabu Bingwa Afrika na Simba Sc kundi A Shirikisho Afrika. Hapo chini ndio mpangilio wa makundi na timu zake. Je, nani kati ya timu zetu za bongo atatoboa kwenda robo fainali? Weka maoni yako kwenye komenti tafadhali.

Hawa Ndiyo Real Madrid Waliowafunga Man City Champions League Jana Usiku

Man City wakiwa wanaongo za kwa 2-1 dhidi ya Real Madrid huku zikiwa zimebaki dakika si zaidi  ya tatu walionekana kama ingekuwa ni timu ya tatu ya Uingereza kuifunga Madrid kwenye uwanja wa Bernabeu. Lakini vijana hao wa Mancini badala ya kuinza kampeni yao kwa ushindi walijikuta wakiachwa nyuma na kuwaangalia Madrid wakiibuka na ushindi baada ya Karim Benzema kusawazisha na kisha Cristiano Ronaldo kufunga goli la tatu na la ushindi, goli lililomfanya bosi wao Jose Mourinho kuslide uwanjani akishangilia goli hilo na Ronaldo. This was the real happiness now from Ronaldo BBC football pundit Robbie Savage alikuwa uwanjani huku Bernabeu. (quoting from BBC SPORTS) "Maicon was not at the races at all in the first half at right-back. He was a passenger and it was like City were playing with 10 men. Cristiano Ronaldo kept coming inside him. "In the second-half, Vincent Kompany looked at what was happening and came across to that wing more. Ronaldo did not...