Mshambuliaji wa zamani wa Chelsea ya Uingereza Didier Drogba ameachwa kwenye kikosi cha timu yake ya taifa ya Cote d'Ivoire kwenye mashindano ya kufuzu kushiriki kombe la dunia katika mechi yao dhidi na Gambia itakayochezwa siku ya Jumamosi.
Drogba ameshindwa kumridhisha kocha wake Sabri Lamouchi baada ya timu hiyo kuondolewa kwenye nusu fainali ya African Cup of Nations na inasemekana kwa mujibu wa Xinhua kwamba mshambuliaji huyo wa Galatasaray inawezekana ukawa ndiyo mwisho wake kuitumikia timu yake ya taifa.
Lamouchi alisema kwamba hajamchagua kwenye kikosi Drogba kwa ajili ya mechi ya Jumamosi kwa sababu anataka kumpa muda wa kufanya mazoezi na kuongeza jitihada ili arudi na kuwa Drogba yule aliyezoeleka zamani.f
Comments