Jeshi la polisi nchini limesema bado linawasaka mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo "CHADEMA" Freeman Mbowe na Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema kufuatia vurugu zilizotokea juzi na madai yao kuwa wanao ushahidi wa kutosha kuhusu polisi kuhusika na kurusha bomu katika mkutano wa Chadema.
Mkuu wa Operesheni ya jeshi na Mafunzo Kamishina Paul Chagonja alisema jeshi la polisi bado linawata Lema na Mbowe wajitokeze hadharani na kutoa ushahidi kwamba polisi walihusika katika kurusha bomu katika mkutano wa Chadema na kusababisha vifo vya watu watatu na jana aliongezeka mwengine na kufikia wanne.
Kamishina Chagonja alisema pia kwa sasa jiji la Arusha ni shwari na watu wanaendelea na shughuli zao bila wasi wasi na kuongeza kuwa endapo Lema na Mbowe hawaliamini jeshi la polisi katika kuwasilisha ushahidi wao, kuna mamlaka nyingi, kuna walinzi wa amani kila mahali, waende hata kwa shehe au hata kwa padre, na kufikia hatua hadi ya kusema kama wana wasi wasi basi waende kwa amiri jeshi mkuu na kumwambia mzee vijana wako hawa hapa na wanatufanyia hiki.
Kamishina Chagonja alisema hali sasa hivi Arusha ni shwari na watu wanaendelea na shughuli zao kama kawaida, watalii wanaonekana kila kona za jiji, magari, akina mama sokoni wanaendelea na kazi zao, hivyo hali ya amani imerudi.
Wakati huo huo wabunge wanne wa Chadema, Tundu Lisu wa Singida Mashariki, Mustafa Akonay na Joyce Nkya wa viti maalum na mwingine mmoja waliachia huru kwa dhamana pamoja na wafuasi wao sitini baada ya kushikiliwa na polisi kufuatia kuhusika na mkusanyiko usio wa halali.
Source: Nipashe Radio One

Comments