Inaonekana watu wameanza kuonea huruma mpiganaji wao Nelson Mandela maarufu kama Madiba baada ya kuendelea kuugua mapafu kwa muda mrefu. Baadhi ya wananchi katika mitaa mbalimbali ya Afrika ya Kusini wameanza kusikika wakitamka maneno ya kuonesha kwamba wanamuaga Raisi Huyo wa kwanza mweusi na mpiganaji dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini humo.
"Mandela ni mzee sana na kwa umri wake, maisha siyo mazuri. Namuomba Mungu amchukue sasa. Ni bora aende. Ni bora akapumzike" Alisikika Ida Mashego, mfanya usafi wa ofisini mwenye umri wa miaka kama 60 hivi huko Johannesburg.
Mtu huyu ambaye ni Artist akichora picha ya
mzee Mandela nje tu ya hospitali
mjini Pretoria alimolazwa Raisi huyo wa
Kwanza mweusi wa Afrika ya Kusini
"Sitadanganya, hali siyo nzuri. Lakini kama nisemavyo, tukiongea naye, anajibu na kujaribu kufungua macho. Bado yupo. Anaweza akawa anaaga lakini bado yupo." Alisema binti yake mkubwa mzee Mandela, Makaziwe, baada ya kumtembelea hospitalini hapo, akiongea na SABC Radio.
Chanzo/source: TVnZ
Comments