Manchester United wanasemekana kumuania Thiago Alcantara ambaye yupo kwenye kikosi cha Hispania cha under 21.
Inasemekana pia kwamba ndani ya Barcelona Thiago ni mkali zaidi ya Xavi na Iniesta kwa umri aliokuwa nao na kiwango alichonacho ukilinganisha na hao wawili na kiwango chao walipokuwa na umri wa miaka 21.
Katia misimu miwili amecheza mechi 81kitu kinachoonesha kuwa mkali zaidi ya hao wenzake, kwani Xavi alicheza mechi 58 ndani ya misimu yake miwili ya kwanza na Iniesta alicheza mechi 29 tu katika misimu yake miwili ya kwanza. Hali hiyo itawafanya Manchester United kujidhatiti kwelikweli kama wanamuhitaji msukuma kandanda huyu.
Comments