Leo Messi hataki kuhusishwa na kuajiriwa kwa kocha mpya Gerardo Martino. "Sihusiki na chochote, na wala sina chochote cha kuelezea. Hayo ni maamuzi ya rais na timu. Kuna wakati nilisema tu kwamba alikuwa ni kocha mzuri lakini sikuwa na chochote cha kuelezea."
"Kibinafsi simfahamu, sijawahi kukutana na yeye wala Luis Enrique ambaye alikuwa katika list ya kuajiriwa. Nadhani ni uteuzi mzuri kwa sababu ataleta kitu cha ziada, na ameonesha uwezo wake kwa Newell na kwa timu ya taifa ya Paraguay. Natumaini atatufaa," aliongeza Messi.
Messi alisema hakukutana na Guardiola kule Munich na kukomenti kwa timu yake: "Tunaanza upya tena baada ya kilichotokea kwa Tito, tunapaswa kujiandaa kwa mwaka mwingine mgumu."
Comments