Meneja mpya wa Man United Daivd Moyes amesisitiza kwamba ana mahusiano mazuri sana na mchezaji wake Wayne Rooney na kuthibitisha kwamba mshambuliaji huyo amerrudi mazoezini akiwa kwenye hali, ari na shape mpya.
Alipoulizwa kama Rooney angebakia United, mskotish huyo aliliambia TalkSport, "Ndiyo, lakini timu imeshasema kwamba Rooney haondoki United, hauzwi. Kuna mengi yamesemwa kuhusu mimi na Rooney miaka ya nyuma, lakini tumekuwa na mahusiano mazuri sana. Wayne ameshakuja nyumbani kwangu nami nimeshaenda kwake pia hivi karibuni kuzungumza naye na sasa tupo wote hapa. Alisema Moyes.
Comments