Amekuwa akihusishwa sana na kutoridhishwa na club yake na kwamba aliamua kupeleka ombi la uhamisho wakati bado United wakiwa chini ya Sir Alex Ferrguson. Na kuna wakati kama vile ilidhihirika wazi kwamba hakuwa na maelewano mema na Ferguson na hata wakati mwingine alimpanga kucheza namba ambayo haikumfurahisha kabisa.
Pia ilisemekana kwamba hata wakati fulani aliwaudhi wachezaji wenzake kwa tabia yake ya kutaka uhamisho.
Jose Mourinho ndiye kocha aliyekuwa anamhitaji sana Wayne Rooney na alishapeleka maombi yake mara mbili, lakni kocha mpya wa United, David Moyes aliyakataa yote. Wakati mpambano wao wa jana ulipokaribia, Mourihno alisikika akisema analiweka swala la kumhitaji Rooney pembeni kwanza ili kungoja mechi yao iishe kwanza. Na baada ya mechi alitangaza kumpa Rooney saa 48 ili afanye uamuzi wake.
Lakini sasa inasemekana pia Rooney ameamua kuachana na mpango wake wa kuondoka Old Trafford.
Je, wewe unadhani Wayne Rooney ataondoka United kwenda Chelsea ama club nyingine?
Comments