Samuel Eto'o amepania kuwaonesha Chelsea na Jose Mourinho kwamba walikuwa sahihi kusitisha usajili wa Wayne Rooney.
Mcameroon huyo ameachana na club yake ya Urusi ya Anzhi Makhachkala na kutia saini kwa mkataba wa mwaka mmoja na kuungana tena na Mourinho, ambaye alikuwa meneja wake walipokuwa Inter Milan.
Wayne Rooney, baada ya kupewa saa 48 na Mourinho ili atoe uamuzi,
jibu lake lilikuwa 'No, nabaki United.'
Mourinho amekuwa akifuatilia mchezaji wa Manchester United Rooney, walakini baada ya kukataliwa mara mbili, Chelsea waliamua kugeukia upande wa pili wa Samuel Eto'o.
"Nilikuwa na nafasi kadhaa za kuja Uingereza hapo awali, pamoja na ile ya kwanza wakati Mourinho alipokuwa hapa, lakini haikuwezekana kwa sababu moja ama nyingine." Alisema Eto'o katika mtandao wa chelseafc.com.
Mchezaji huyo wa zamani wa Barcelona hajasafiri na Chelsea kwenye mchuano wa European Super Cup dhidi ya Bayern Munich - yeye wala Willian, ambaye uhamisho wake toka Anzhi ulithibitishwa siku ya Jumatano iliyopita.
Eto'o atapaswa kusubiri hadi international break ndipo aanze kuonekana uwanjani, watakapokuwa ugenini kupambana na Everton September 14.
Uhamisho wake huo inaonekana usingefanyika endapo Mourinho angekubaliwa kumchukua Rooney.
Mourinho alisema: "niliwaambia niliyopaswa kusema, nadhani niliweka wazi sana hatukupeleka ombi la tatu, hatuna zaidi cha kusema, Rooney ni mchezaji wa Man United na hakuna cha ziada."I
Kumpata Eto'o, ambaye imelipotiwa kuwa alikuwa akilipwa £300,000 kwa wiki huko Urusi, ni kinyume na taratibu za Chelsea za kusaini wachezaji vijana. Hali hii pia inaacha swali juu ya mustakabali wa Demba Ba and Fernando Torres kwani Mourinho ameweka wazi kwamba kuwa na washambuliaji wanne ni too much na kufunguka kwa kusema kuwa Romelu Lukaku ndiye tegemeo la badaye kwa Chelsea.
Nafasi ya Ba kwenye kikosi hicho ipo hatarini, lakini Torres bado anahitaji kulipa £50million kwa Liverpool, kama Mourihno alivyoweka wazi mapema wiki hii.
Comments