Manchester United hatimaye wamekamilisha usajili wa Mchezaji toka Everton, Marouane Fellaini kwa donge la £27.5m. Inasemekana kwamba Fellaini mwenyewe ana furaha sana kujiunga na mashetani wekundu hao kutoka jiji la Manchester, na kwamba yupo tayari kufunga magoli mengi iwezekanavyo ili kulipa fadhila za kocha wake mpya David Moyes.
Haya ndiyo aliyoyaongea Fellaini mwenyewe kuhusu usajili wake:
'It’s a big moment for me,'I waited for a long time, I’ve worked hard for this and I’m very happy to join this great club. It’s the biggest club in the world… I tried everything to join. It’s been difficult, a very long day. I waited to the end… I know the situation, but this day has been very long. I hope I can score a lot of goals for Manchester United.When I was young it was a dream to play for Manchester United. Now I’m here so I’ll try to give my best to the club. I want to win trophies. That’s the most important thing.
Kwa mujibu wa meneja David Moyes, Fellaini atacheza sehemu ya kiungo na siyo nyuma ya Robin Van Persie kama wengi walivyotarajia.
Gareth Bale naye alikamilisha uhamisho wake toka Tottenham Hotspurs kwenda Real Madrid ya Hispania na kumnya acheze soka lake kwa karibu sana na Cristiano Ronaldo. Naye inasemekana amefurahi sana kupata ya kucheza na Ronaldo.
Ozil naye hatimaye alikamilisha usajili wake na The Gunners wa London na sasa n mchezaji wa Arsenal.
Comments