Hii ni jana majira ya kuanzia saa tisa hivi alasiri wakati wa mpambano mkali wa kukata na shoka kati ya Liverpool na Manchester United wa Premier League ya kule Uingereza. Ambapo Liverpool waliweza kuutumia uwanja wao wa nyumbani kwa kuwachabanga Man United 1-0. Goli ambalo lilifungwa na Sturidge kunako dakika ya 3 tu ya mchezo huo, na goli hilo kudumu hadi mwisho wa mchezo.
Hapa Arusha kumekuwa na msemo miongoni mwa washabiki wa Liverpool aka "You will never walk alone" kuwa goli linalofungwa na mshambuliaji wao machachari sana aliyesajiliwa msimu uliopita kutokea Chelsea Sturidge hua halisawazishwi na kwamba pindi anapofunga goli tu wana uwezo wa kumtoa golikipa wao ili goli libaki wazi kwani hakuna timu yenye uwezo wa kusawazisha goli lake. Msemo huo sasa ulitimia kwa mashabiki wa Man United ambao walidhani ni mzaha mzaha tu na kwamba wakati wowote timu yao ingesazisha bao hilo. lakini wapi.....! Basi hadi mwisho wa matanange huo Liverpool 1, Man United 0. Hongera kwa Liverpool...! It was a good soccer you showed with good winning spirit...!
Hapa chini nimekuwekea picha za mashabiki wa mechi za jana walipokuwa wakifuatilia mipambano hiyo kwenye club moja inayoonesha Ligi ya Uingereza kpitia DSTV... CR PUB-ARUSHA njia ya kwenda Moshono.
mashabiki wa Man United na Liverpool wakifuatilia mpambano
mashabiki wa Man United na Liverpool wakifuatilia mpambano
Huyu ni mshabiki machachari sana wa Arsenal kwa jina ni Erasto Martin na jana alikuwa
ni mwenye furaha sana baada ya timu yake kuwafunga Spurs 1-0.
Huyu ni mshabiki machachari sana wa Arsenal Erasto Martin
akiwa amekaa na mshabiki wa Man United maarufu kama Munasiju mara baada ya
United kufungwa na mechi yao kuisha
Munasiju, shabiki nguli wa Man United akifwatilia mpambano
Huyu hapa ni shabiki wa Liverpool akiwa amestarehe akiamini
kwamba goli la Sturidge halirudishwagi.
Huyu ndiyo alikuwa kituko kabisa. Kwanza alikuwa kalewa,
pili alikuwa anashabikia kwa nguvu zote timu yake ya Arsenal
na kuwabeza Man United kwamba watakapo kutana nao wajiandae kwa kipigo kikali.
Comments