Manchester United wanajipanga kutoa ofa ya mkataba mnono kwa kiungo wake mchanga na machachari Adnan Januzaj, mkataba ambao utampatia mshahara wa £60,000 kwa wiki. Aliripoti Colin Young wa The Daily Mail huko majuu. .
Januzaj, 18, kwa mara ya kwanza alicheza muda wa kutosha kwa timu yake ya Red Devils mwishoni mwa wiki iliyopita, akiwa amejiunga na timu akitokea Anderlecht mwaka 2011. Magoli yake yakiipatia United ushindi wa 2-1 walipokuwa ugenini wakikipiga na Sunderland, ingawaje, club yake wana hamu sana ya kuweka naye mkataba mpya kwani mkataba wake wa sasa utafikia kikomo kipindi kijacho cha cha majira ya joto .

Comments