Unataka Kujua Samuel Eto'o Amesema nini Kuhusu Soka la Uingereza? Je, kwa nini Jose Mourinho Anamlaumu? Bofya tu Hapa Uyapate Yote Hayo.
Eto'o mwenye miaka 32, ambaye ameshachezea Real Mallorca, Barcelona na Inter Milan miaka ya nyuma, alipewa kipaumbele cha kuanza kikosi cha kwanza na Meneja wake Jose Mourinho, lakini ametupwa kwenye benchi baada ya kushindwa kumuimpress.
Mourinho amelaumu kiwango cha chini cha Eto'o kwani alitumia miaka miwili akicheza ligi ya chini ya Urusi akiwa na timu ya Anzhi, lakini mkameruni huyo ameonesha kutokupaniki na ana hakika atarudi kwenye kiwango cha juu.
Alisema yafuatayo kwa Chelsea Magazine: “Tayari nimetambua kuwa mpira wa England ni wa nguvu sana - ni wa kutumia nguvu zaidi ya aina nyingine za mpira.
“Sijapata muda mwingi bado, hivyo nahitaji kuendeleza bidii kuhakikisha kiwango kinakua. Kila mchezo hapa ni muhimu na ninatambua kwamba nimekuja hapa kufurahia kuichezea Chelsea na kurahia mpira. Kila mchezo nauendea kwa mtindo huo.
“Haijalishi unanichezesha sehemu gani, nitacheza mpira. Wenzangu wananisaidia sana hata kocha pia, hivyo najihisi kuwa nakaa vizuri kwenye timu."
Comments