Leo ndiyo leo, asemaye kesho ni mwongo! Waswahili hunena kauli kama hiyo pale jambo kumbwa hususan lenye kufurahisha linapotazamiwa kutokea.
Watu wengi sana hupenda mpira wa miguu almaarufu kandanda, kabumbu kwa wabongo, football ama soccer kwa wenzetu wa USA na kule England. Basi leo ndiyo siku ambayo wengi wamekuwa wakiingojea kwa hamu kubwa sana, siku ya ufunguzi wa mashindano ya fainali za Kombe la Dunia litakaloshindaniwa kuanzia usiku wa leo, saa tano kwa Afrika Mashariki huko Brazil, Amerika ya Kusini.
Katika mechi ya ufunguzi leo, wababe wawili ama majogoo wawili Brazil na Croatia watamenyana vikali sana kama si kuumana na kuzifanya zil nyasi za mandia au kapeti lile kupata shida sana kwa kipindi cha dakika 90 zote.
Je, nani ama timu ipi itaibuka kidedea leo?

Comments