Skip to main content

Kama Kawaida http://abelrk.blogspot.com Inakuletea Matukio ya Mechi za jana FIFA World Cup Quarter Final. Hapa ni Brazil v Colombia.

Brazil 2 {{Thiago Silva na David Luiz}} v Colombia 1 {{James Rodriguez}}

Angalia haya ndiyo matukio ya mchezo wao wa jana ambapo Brazil walihakikisha kwamba sio tu wanajenga heshima toka kwa Colombia bali pia wanatinga fainali. Pia alithibitisha kwamba mapungufu yao kama yalivokuwa yakizungumzwa na wachambuzi wengi wa soko si kweli na kwamba wao hubadilika kutokana na mchezo.


 Alikuwa ni Thiago Silva aliyewaweka Brazil mbele baada
ya kuunganisha free-kick iliyochongwa kwa ufundi na Neymar JR


Ikumbukwe kuwa Brazil na Colombia walikutana jana katika World cup kwa  mara ya kwanza katika historia ya kombe la dunia. Colombia, timu ambayo inasifika sana kwa mchezo wa kasi na mashambulizi ya mara kwa mara wakiongongozwa na James Rdriguez ilikuwa ni timu ngumu sana kufungika lakini jana walikutana na kisiki Brazil ambao walijiimarisha sana hasa sehemu ya kiungo huku wakitumia vizuri sana wings zao ambazo zilikuwa zinapeleka mashambulizi mazuri, ya nguvu na ya mara kwa mara.



Baadaye akafwata David Luis aliyeipatia Brazil goli la pili baada ya
 kupiga mpira wa adhabu na kutinga moja kwa moja nyavuni huku kipa
wa Colombia akishindwa kabisa kuuzuia.

 David Luiz katika staili za kushangilia goli la ushindi

Baadaye Colombia walifanya mashambulizi ya kuua mtu na baada ya kipa wa Brazil kuona ameshapitwa basi hakuwa na jinsi zaidi ya kumfanyia madhambi mchezaji wa Colombia na Refa kuamuru ipigwe penati. Alikuwa si mwingi ba ni yule anayeongoza kwa kuwa na na magoli sita sasa kwenye fainali hizi James Rodriguez aliyepiga penati hiyo kwa ufundi na kuandika goli pekee kwa Colombia.


 Huu ndiyo umma wa wabrazil waliojitokeza kuhakikisha wanashangilia
hadi timu yao inaibukwa na ushindi.

 Huku shabiki huyu wa Colombia akilia baada ya timu yake
kupigwa 2-1 hapa chini mashabiki hawa wa Brazil wapenzi hawa
wakishangilia kwa mtindo wa pekee kwa busu la upendo kati yao na ule wa nchi yao.
Furaha iliyoje!

Baada ya hapo Colombia walijaribu kuhamia langoni mwa Brazil huku wakifanya mashambulizi ya hatari sana lakini bahati haikuwa yao kwani walinzi wa Brazil walijiimarisha kuhakikisha hakuna dakika za nyongeza zinaongezwa ili kumsaka mshindi.





 Colombia waliendelea kujaribu bahati yao bila mafanikio
 Rodriguez akiwa haamini kama matokeo ya mechi ni Brazil 2 v Colombia 1
 Hapa chini ndipo Neymar alipomalizwa kabisa baada ya kuchezewa
 madhambi mabaya sana huku refa akiamuru mchezo uendelee
 akiwapa Brazil advantage kwani walikuwa na mpira bado. Neymar
alipigwa kwa goti sehemu yake ya mgongo na kumfanya ashindwe
 kuinuka kabisa na hatimaye kupelekwa nje kwa machela.

 Picha ya chini jamaa wa Colombia akipachika bao wakati mchezaji
mwenzake akiwa ameotea na goli lake lilikataliwa na refa.

Moja ya matukio ya kusikitisha sana kwa Brazil ni kuumia kwa Neymar JR ambapo kutamfanya azikose mechi zilizo salia za nusu fainali na ile ya fainali endapo watamfunga Germany. Angalia picha hapo chini.








Brazil watakutana na Germany katika mechi yao ya nusu fainali. Je, kwa mtazamo wako, Brazil watatoka kwa Germany? Usisite kutoa maoni yako tafadhali.


Comments

Popular posts from this blog

These are Said to Be the Best Goalkeepers in the World, Ranking from 1-25

25. Stephane Ruffier, Saint-Etienne Had Stephane Ruffier not sustained a groin injury in 2011, Monaco might never have been relegated to Ligue 2. But he did, and they were, and that summer the then-24-year-old goalkeeper joined Saint-Etienne, rebuffing Manchester City in the progress. This season he played all 38 Ligue 1 matches for Les Verts for a second season in succession, conceding just 32 goals as his side finished a surprising fifth in the standings and qualified for the Europa League. 24. Pepe Reina, Liverpool Only Joe Hart kept more Premier League clean sheets than Pepe Reina in 2012-13. In a season that saw Liverpool finish a disappointing seventh in the English top-flight, the 30-year-old managed to keep things respectable from a defensive standpoint, conceding only 34 goals and stopping 88 per cent of the shots he faced. To finish the season he conceded just a single goal in his last four matches. 23. Mariano Andujar, Catania Only Parma managed ...

Hawa Ndiyo Real Madrid Waliowafunga Man City Champions League Jana Usiku

Man City wakiwa wanaongo za kwa 2-1 dhidi ya Real Madrid huku zikiwa zimebaki dakika si zaidi  ya tatu walionekana kama ingekuwa ni timu ya tatu ya Uingereza kuifunga Madrid kwenye uwanja wa Bernabeu. Lakini vijana hao wa Mancini badala ya kuinza kampeni yao kwa ushindi walijikuta wakiachwa nyuma na kuwaangalia Madrid wakiibuka na ushindi baada ya Karim Benzema kusawazisha na kisha Cristiano Ronaldo kufunga goli la tatu na la ushindi, goli lililomfanya bosi wao Jose Mourinho kuslide uwanjani akishangilia goli hilo na Ronaldo. This was the real happiness now from Ronaldo BBC football pundit Robbie Savage alikuwa uwanjani huku Bernabeu. (quoting from BBC SPORTS) "Maicon was not at the races at all in the first half at right-back. He was a passenger and it was like City were playing with 10 men. Cristiano Ronaldo kept coming inside him. "In the second-half, Vincent Kompany looked at what was happening and came across to that wing more. Ronaldo did not...

MANCHESTER UNITED VS CHELSEA #EPL TODAY AT OLD TRAFFORD STADIUM

MANCHESTER UNITED vs CHELSEA FC LEO #EPL USIKOSE NA USIKUBALI KUSIMULIWA #TheBattleAtOldTrafford:  Jioni ya leo miamba ya kabumbu la Uingereza inakutana katika mpambano unaotarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua. Manchester United leo wanawakaribisha mahasimu wao Chelsea pale Old Trafford kwenye mchezo wa round ya pili ya Premier League. Ikumbukwe kuwa Katika mchezo wa kwanza walipokutana pale Stamford Bridge Chelsea waliwanyuka Man United 1-0,  goli lililofungwa na Alvaro Morata kwa kichwa. Kuna kama kauadui flani hivi kati ya makocha Antonio Conte wa Chelsea na José Mourinho wa Man United. Na huu ni uhasimu ambao kila mmoja wao anajaribu kuuficha na kuonesha kuwa hawana shida kati yao. Mourinho amenena kuwa game kati ya timu hizi mbili ni ya kawaida kwake kama game nyingine nyingine na hakuna chochote special kuihusu. Lukaku, Rashford, Martial,  Matic,  Pogba, De Gea  na wengineo wanategemewa kuongoza kikosi cha man United leo huku Morata, Fabregas, Pe...