Kama Kawaida http://abelrk.blogspot.com inakuletea Matukio ya FIFA World Cup Quarter Final kati ya German v France.
German 1 (Hummels) v France 0
Katika mchezo ambao ulikuwa mgumu sana kutabiri kwamba nani angeibuka kidedea Ujerumani walijidhatiti vilivyo na kufanikiwa kuwazima Ufaransa mapema sana na baadaye kulishikilia goli lao hilo hata mwisho wa mpambano.
Ilimbidi kipa wa Ufaransa kuudaka mpira ukiwa tayari umeshatinga nyavuni.
Pamoja na kwamba Ufaransa walijitahidi sana kulishambulia goli la Ujerumani mara kwa mara wakitafuta goli angalao la kusawazisha huku wakimtumia mshambuliaji wao hatari sana Benzema lakini walinzi wa Ujerumani walikuwa imara sana wakiongozwa na golikipa waoa mbaye hakutaka kabisa mchezo ama utani langoni mwake. Hivyo mwisho wa dakika 90, Ujerumani 1 v Ufaransa 0.
Wachezaji wa Ujerumani wakishangili goli lao lililopachikwa nyavyni na Mats Hummels
Ujerumani wametinga nusu fainali ambapo watakuwa na kibarua kikali pale watakapo pepetana na Brazil ambao waliwapelekeha mchakamchaka Colombia na kuwafurumusha nje ya mashindano kwa ushindi wa 2-1.
Benzema alijaribu mara kadhaa kutaka kuisawazishia
timu yake basi hata waende dakika 120 lakini hali ilizidi kuwa
tete kwa Ufaransa. Basi akawa hana namna zaidi ya kuyapokea
matokeo kwa mikono miwili na bila hiyana.
Hali si hali..... Unaambiwa hali ni tete....
Huwezi amini jamaa wanakubali matokeo na kwenda kufungasha
virago kurudi home ama kitaa.
Pogba naye alijaribu kila liwezekanalo kama ilivyo kawaida
yake lakini wapi. Hali haikuwa hali kwa upande wao.
Wakasalimu amri na kuwa wateja wa Ujerumani.
Wachezaji wa Ufaransa wakafanya kama wengine ambavyo wangefanya,
nayo ni Kujifariji na kufarijiana wao kwa wao. Kwani wahenga walinena,
'asiyekubali kushindwa si mshindani.'
Ujerumani sasa watavaana na Brazil katika hatua ya nusu fainali. Je, watatoka kwa wazee wa SAMBA?
Comments