Leo ni mchezo mwingine tena ambao unamfanya bosi wa Old Trafford Louis Van Gaal kutazamwa na mashabiki wengi wa soka hapa bongo na pande zingine za dunia.
Baada ya United kupoteza mechi ya kwanza ya ufunfuzi dhidi ya Swansea kwa kichapo cha 1-2 huku tatizo Kubwa likiwa upande wa ulinzi. Pia katika mechi ya pili walilazimishwa sare ya 1-1 dhidi ya Sunderland.
Leo wakiwa wanategemea kuwaanzisha wachezaji wawili waliosajiliwa hivi Karibuni Marcos Rojo pamoja mvunja rekodi ya usajili ulaya Angel Di Maria, United watafanya kila liwezekanalo ili kushinda mechi ya Leo ili kuwarisha mabosi wao Van Gaal na Giggs pamoja na uongozi mzima wa United bila kusahau kwamba itakuwa ni faraja kubwa sana kwa mashabiki wao kwani wamekuwa ni watu wa kutaniwa tu kila kukicha.
Di Maria anatarajiwa kuongoza safu ya kiungo huku akipeleka Pasi nyingi kwa mastraika Wayne Rooney na Van Persie na wakati mwingine akifanya mambo yake mwenyewe. Marcos Rojo anatarajiwa kuongoza safi ya ulinzi akisaidiana na akina Jones, Evans pamoja na Valencia ambaye huenda akarudishwa nyuma Leo kutokana kuumia kwa Smaling kwenye mechi iliyopita.
Barnley wenyewe pia sio timu ya kubeza kwani ndio wamepanda daraja msimu huu na hawangetaka kupoteza mchezo kirahisi sana.
Basi tungoje dakika tisini ili ziamue nani mshindi leo.
Je, United watashinda au wataendeleza ukibonde?
Comments