Mechi kati ya Liverpool dhidi ya Manchester City ni moja ya mechi zenye mvuto mkubwa kwa mashabiki wa soka katika ligi kuu ya Uingereza almaarufu kama 'Barclays Premier League ama EPL yaani English Premier League.
Ukizitazama timi hizi mbili utaona kwamba zote mbili zina uwezo mkubwa wa kushinda mechi ya Leo itakayopigwa usiku majira ya SAA NNE kwa saa za Afrika Mashariki.
Liverpool wana striking force yao imara sana ikiongozwa na Sturridge pamoja na Sterling na kwa sasa wakiwa wanakamilisha usajili wa mtukutu Mario Baloteli ambaye haijafahamika kama atakipiga leo ama vipi. Kwa upande wa Man City wanategemea sana mastraika kama akina Aguero, Silva na wengineo kuhakikisha wanalizamisha jahazi la Majogoo.
Ukifwatilia maoni ya mashabiki wa soka wengi hutoa nafasi kwa majogoo kutwaa pointi tatu huku wachache sana wakiipa nafasi timu ya vijana toka Etihad Stadium.
Wapi unatupa karata yako ya ushindi?
Comments