Baada ya kuchezea kichapo cha magoli 2-1 wakiwa nyumbani kwako Old Trafford, Manchester United maarufu kama Red Devils jumapili hii watakuwa wageni wa Sunderland katika mechi nyingine ya Premier League kule Uingereza. Mechi hii pia itatazamwa na wengi kama mtihani mwingine kwa kocha Louis Van Gaal. Wengi wanampa kocha huyu imani lakini wakitilia shaka kikosi alichonacho. Wengi pia wanatumaini kuwa atafanya usajili nzuri kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili hapo Agosti 31.
Van Gaal ameshasajili akina Herrera, Shaw pamoja na beki mwingine Marcos Rojo ili kuimarisha kikosi chake.
Ikumbukwe pia Sunderland waliwachapa United katika mechi ya mwisho ya msimu uliopita na kuepuka kushuka daraja wakati United wakiwa chini ya kocha mchezaji Ryan Giggs baada ya David Moyes kufungashiwa virago pale ilipoonekana alishindwa kuvaa viatu vya SAF aliyestaafu.
Je, United watashinda mechi ya kesho? Wasiposhinda unadhani watu ama wanahabari za soka watasemaje?
Comments