Manchester united leo wamerudi katika ligi baada ya ukame wa ushindi katika mechi tatu mfululizo ambapo walifungwa game ya kwanza 1-2 na Swansea, wakienda sare na Sunderland ya 1-1 na sare nyingine ya 0-0 dhidi ya Barnley.
Leo wamefanya kufuru baada ya kuwafurumusha bila huruma vijana wa QPR kwa kuwalambisha mabao 4-0 katika dimba lao la Old Trafford.
Wafungaji
1. Di Maria
2. Herrera
3. Rooney
4. Mata
Huku United wakiwatumia kwa Mara ya kwanza Rojo, Herrera na Falcao na Blind. Kikosi kilikuwa imara kiasi kwamba ilifanya game kuwa rahisi sana kwa United kuzoa pointi zote tatu.
Comments