Hayo yalitokea baada ya nyota Frank Lampard kuifungia timu yake mpya ya Manchester City bao la kusawazisha dhidi ya timu yake ya zamani Chelsea wakati miamba hiyo ilipovaana katika mpambano mkali wa Premier League mule Uingereza siku ya Jumapili iliyopita.
Lampard akicheza kwa mara ya kwanza dhidi ya timu aliyoichezea kwa takribani miaka kumi na tatu, alifunga bao hilo zikiwa zimesalia dakika chache sana mpira uishe. Huku goli la Chelsea likikwamishwa na Andre Schurrle katika dakika ya sabini.
Lampard alishangiliwa na mashabiki baada ya mechi maisha hasa wale wa Chelsea lakini Mourinho alionekana kununa pale alipoulizwa kuhusu mapenzi ya Lampard kwa Chelsea.
"Lampard ni mchezaji wa Manchester City, alipoamua kwenda kwenda timu pinzani basi swala la mapenzi limeishia hapo. Kumwongelea Frank ni kuongelea maisha yangu ya zamani na Frank." Hayo baadhi tu ya maneno aliyobwabwaja Mourinho siku hiyo.
Brings You Global News!
Comments