Hatimaye Mh Edward Ngoyai Lowasa ametangaza kuwania urais kwa tikiti ya chama tawala cha CCM mbele ya umati wa wakazi wa jiji LA Arusha uliokusanyika kumsikiliza.
Watu walianza kukusanyika uwanjani hapo mapema sana asubuhi wakisubiri mzee huyo kwa hamu kusikia akitangaza azma yake hiyo huku wakitumbuzwa kwa burudani nyingi toka kwa wasanii mbalimbali wa kitanzania.
Unaweza kushuhudia mwenyewe kupitia picha hizo jinsi watanzania walivoitikia wito wake kufika uwanjani hapo wakiwemo waandishi wa Habari, wasanii mbalimbali, wachungaji, mashehe, maaskofu, manabii na mitume, viongozi mbalimbali wa CCM toka mikoa mingine akiwemo mwenyekiti wa CCM Geita anayejulikana kwa jina la MSUKUMA ambaye alitua uwanjani hapo kwa helikopta akitokea Geita.
Wananchi walionesha kuvutiwa na kuipenda sana kauli aliyoitoa ya ''Maamuzi Magumu'' kwani kila alipotamka hivo tu umati ulipiga shangwe na mayowe kushangilia. Kauli ya pili iliyopendwa sana ni ili kauli mbiu yake ya mbio za urais inayosema ''Safari ya Matumaini, Inaanza Leo''. Na imekwishaanza tangu Jana tarehe 30/05/2015. Mungu ibariki Tanzania, Mungu wabariki wagombea, Mungu tuchagulie kiongozi shupavu na anayeipenda nchi yetu. Amina!
Comments