Lejendari wa kandanda kutoka Brazil Dunga ambaye ni kocha wa Kikosi
cha Brazil amedai kwamba hataki kuwatetea wachezaji wake wa Brazil mara
baada ya kutolewa mashindanoni walipokwaana na Paraguay walipokuwa
wakisaka kutinga nusu fainali ya michuano ya Copa Amerika lakini
alithibitisha kuwa chanzo kimojawapo cha wao kufungwa ni kwamba ndani ya
hiyo wiki ya game baadhi ya wachezaji wa Brazil walikumbwa na virusi.
"Siyo kwamba nawatetea, hapana! Lakini wachezaji wangu 15 walikumbwa na virusi wiki ya kuelekea match day na hivyo kunifanya kutowapatia baadhi ya mazoezi kwenye maandalizi ya mechi" alisema Dunga.
"Siyo kwamba nawatetea, hapana! Lakini wachezaji wangu 15 walikumbwa na virusi wiki ya kuelekea match day na hivyo kunifanya kutowapatia baadhi ya mazoezi kwenye maandalizi ya mechi" alisema Dunga.
"Wachezaji waliumwa na kichwa, mgongo na homa. Wengine waliumwa zaidi
ya wengine, nikapaswa kupunguza umakini wa mazoezi ili waweze kupona.
Wengine walitapika kabisa" alisema tena na kuongeza kwamba, "Wllian
aliumwa wakati wa half time na Robinho aliumwa mwishoni mwa mechi."
Waliandika #LiveScorer
Comments