Middlesbrough walipata bahati ya kuzipatia penati, alisema meneja wa Manchester United Louis van Gaal. Aliyasema hayo baada ya timu yaku kutupiliwa virago nje ya mashindano ya League Cup na mabingwa hao siku ya Jumatano.
Keteni Wayne Rooney, Michael Carrick na Ashley Young wote walikosa penati na kufanya kuchukua kichapo cha 3-1.
"ni kama kasino vile, nyekundu ama nyeusi. Walikuwa na bahati lakini kiukweli unaweza kuilazimisha bahati ikupate. Jana tulifanya mazoezi ya penati, lakini ndiyo hivyo. Siwawezi hawa." Van Gaal aliwaambia waandishi wa habari.
United wamepoteza mechi tatu kati ya nne za mwisho za League Cup pale walipokutana na wapinzani wa ligi ya chini na Van Gaal amewalaumu vijana wake kwa kutokuwa na umaliziaji mzuri, hasa baada ya kukosa nafasi nyingi sana Jumatano.
"Ndhani tulikaribia sana, na tulipaswa kushinda kwa sababu tulitengeneza nafasi nyingi sana, hasa kipindi cha pili na dakika za nyongeza." alisema kocha wa United na meneja wa zamani wa Uholanzi.
"Tulipata nafasi kutoka mita moja, mita mbili mbele ya goli."
Mlinzi Chris Smalling amewaomba wenzake kupandisha kiwango pale watakapotembelea Crystal Palace Jumamosi, ambao wamepoteza mechi zao tatu za mwisho katika Premier League.
"Kila mmoja amenyong'onyea chumbani. Tulipata nafasi nyingi sana lakini haikuwezekana." Smalling alisema katika website ya United (www.manutd.com).
Comments