Mkali, mkongwe na Lejendari wa muziki aina ya hiphop Joseph Haule alimaarufu kama Professor Jay ameibuka kidedea katika uchaguzi wa jimbo la Mikumi kupitia tikiti ya Chadema-Ukawa.
Mwimbaji huyo wa kufokafoka, ambaye hadi sasa ana albamu tano, alimdunda mpinzani wake kwa kishindo sana katika uchaguzi uliofanyika Jumapili 26 Oktoba 2015 .
"Siko hapa kwa ajili ya kuwaongelea wasanii tu bali na watu wa Mikumi pia. Baada ya hili natarajia kuteuliwa na serikali kuwawakilisha watu wangu vizuri zaidi. . . labda katika nafasi ya uwaziri ama kitu kingine. Kwa hiyo nitakuwa mwanamuziki wa kufokafoka wa kwanza kuwa waziri Afrika Mashariki. Jay aliwaambia wana habari baada ya ushindi wake kutangazwa.
Mh. Joseph Haule alimaarufu kama Professor Jay

Jay alipata kura 32,259 dhidi ya 30,425 za mpinzani wake wa CCM Jonas Nkya.
"Tumeshinda kwa tofauti ya kura 1,834 . Asante Mungu na watu wa Mikumi kwa kuniamini," Alitupia hiyo kwenye mtandao wake wa kijamii kuthibitisha ushindi wake.
Jay alianza muziki mwaka 1994 akiwa kama mwanachama wa kundi la Hard Blasters, kabla ya kuamua kuwa solo artist 2001. Baadhi ya nyimbo zake maarufu ni kama vile Nikusaidiaje and Zali la Mentali.
Comments