Skip to main content

Wingu Zito Lafunika Uchaguzi Tanzania!

Uchaguzi wa Tanzania uliingia mashakani siku ya Jumatano tarehe 28/10/2015baada ya tume ya uchaguzi Zanzibar kutangaza kwamba uchaguzi huo ulivurugwa.

 Bwana Seif Sharif Hamad wa CUF anayedaiwa kujitangaza kushinda urais visiwani Zanzibar

Upande wa upinzani pia wamepinga utangazaji wa matokeo ya uchaguzi huo uliofanyika siku ya Jumapili 25/10/2015 ambao umeshuhudiwa CCM wakipata upinzani mkali sana katika historia ya uchaguzi hapa Tanzania. 

Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar ilsema siku ya Jumatano kuwa uchaguzi uliofanyika Visiwani humo ambao ulikuwa na wapiga kura wapatao laki tano walioandikishwa waliopigia kura serikali ya Zanzibar na ilie ya Muungano kuwa ni lazima urudiwe wakidai kuwa uchaguzi ulivurugwa. 

"Utaratibu haukuwa wa haki na sheria zilivunjwa . . . hivyo natangaza kwamba matokeo yote kuwa batili," alisema mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Zanzibar Bwana Jecha Salim Jecha said.

Siku ya Jumatatu kiongozi wa upinzani katika mbio za urais kwa Zanzibar Seif Sharif Hamad alijitangaza kuwa mshindi kabla ya tangazo rasmi la tume. 

Katika majimbo 264, 133 yameshatangazwa matokeo yake huku Hohn Pombe Magufuli wa CCM akiwa  ameshinda kwa asilimia 56.51 ya kura na Edward Lowassa wa Chadema akipata asilimia 41.67 ya kura, tume ya taifa ya uchaguzi iltangaza siku ya Jumanne.

Lakini wakati CCM wakiwa mbele kwenye mbo hizo za urais, mawaziri vigogo wamepoteza viti vya ubunge. 

Ulinzi ulitawala Zanzibar hasa maeneo ta kutangazia matokeo baada ya Sif Sharif Hamad wa CUF alipotoa onyo kuwa "asingekubali kushindwa iwapo angeibiwa kura." 

Wachambuzi na waangalizi wa uchaguzi wameonya kuwa upinzani mkali ulipo kwa sasa unaweza kusababisha ghasia, huku wapinzani kwa mara ya kwanza wakito upinzani mkali kwa CCM haijawahi kutokea tanga kuanzishwa kwa demokrasia mwaka 1995. 

Watazamaji wa kimataifa wa uchaguzi nchini Tanzania waliusifu mfumo wa upigaji kura siku ya Jumapili. "Ingawaje kulikuwa na matatizo madogo madogo kwenye baadhi ya vituo, lakini picha ya jumla inaonesha kila mtu alipata nafasi ya kupiga kura kwa uhuru na kwenye mazingira mazuri na ya amani," alisema Judith Sargentini, ambaye ni European Union election observer chief,

Mkuu wa waangalizi wa African Union Commission chief Nkosazana Dlamini-Zuma naye ameisifu Tanzania kwa jinsi walivyoendesha zoezi zima la uchaguzi, lakini pia aliwaonya wagombea "kuweka nchi yao mbele ya mambo mengine yote". Rais anayemaliza muda wake Dr. Jakaya Kikwete ameiomba polisi kutia nguvu katika suala la ulinzi kuhakikisha utulivu unakuwepo. 

Comments

Popular posts from this blog

MAKUNDI CHAMPIONS LEAGUE NA SHIRIKISHO AFRIKA

Yanga Sc kundi A Klabu Bingwa Afrika na Simba Sc kundi A Shirikisho Afrika. Hapo chini ndio mpangilio wa makundi na timu zake. Je, nani kati ya timu zetu za bongo atatoboa kwenda robo fainali? Weka maoni yako kwenye komenti tafadhali.

Hawa Ndiyo Real Madrid Waliowafunga Man City Champions League Jana Usiku

Man City wakiwa wanaongo za kwa 2-1 dhidi ya Real Madrid huku zikiwa zimebaki dakika si zaidi  ya tatu walionekana kama ingekuwa ni timu ya tatu ya Uingereza kuifunga Madrid kwenye uwanja wa Bernabeu. Lakini vijana hao wa Mancini badala ya kuinza kampeni yao kwa ushindi walijikuta wakiachwa nyuma na kuwaangalia Madrid wakiibuka na ushindi baada ya Karim Benzema kusawazisha na kisha Cristiano Ronaldo kufunga goli la tatu na la ushindi, goli lililomfanya bosi wao Jose Mourinho kuslide uwanjani akishangilia goli hilo na Ronaldo. This was the real happiness now from Ronaldo BBC football pundit Robbie Savage alikuwa uwanjani huku Bernabeu. (quoting from BBC SPORTS) "Maicon was not at the races at all in the first half at right-back. He was a passenger and it was like City were playing with 10 men. Cristiano Ronaldo kept coming inside him. "In the second-half, Vincent Kompany looked at what was happening and came across to that wing more. Ronaldo did not...