Ni ngumu kuamini lakini ukweli siku zote unabaki kuwa ukweli kwa sababu kuu moja tu kwamba jambo limetokea na watu wamelishuhudia.
Nilipokuwa nikisikiliza maneno toka kwa mashabiki wa Arsenal na matambo yao kwamba wanapanda kileleni kwa kuwa na uhakika kuwa wangemtwanga Southampton ilinifanya kuamini kwani niliona ni jambo linalowezekana sana.
Lakini waswahili husema "mpira wadunda" wakimaanisha kwamba lolote laweza kutokea.... yaani ukweli waweza kuwa uongo na uongo kuwa ukweli.
Sijui kwa nini nazunguka sana hivi.. ni kwamba mechi ya EPL ya late night yaani usiku mwingi ya jana matokeo yapo hivi na hayawezi futika wala mechi haiwezi kuahirishwa kwani kilichotokea ni halali. Southampton 4-0 Arsenal...
Nimewajibika tu ku post....
Pia mechi nyingine iliiisha hivi.
Newcastle 0-1 Everton.
Comments