Skip to main content

Rais JPM Awa Gumzo Duniani..

Hivi sasa baadhi ya marais wa nchi mbalimbali wameanza kusifia jihudi, maarifa na kasi ya rais wa awamu ya tano ya Tanzania Dr. John Pombe Magufuli.
JPM tangu aingie madarakani takribani mwezi mmoja amekuwa akifanya juhudi za dhati za kuikomboa nchi toka kwa mapapa ya ufusadi akianzia wizara ya fedha, bandari, TRA na sehemu nyingine akiwawajibisha wala rushwa, wakwepa kodi na wahujumu uchumi wa nchi huku wengine vibarua vyao vikiota nyasi na wengine hata kupelekwa mahakamani kujibu mashtaka.
JPM alionekana leo ktk mtaa wa feri DSM akifanya usafi na majirani zake akitii amri aliyoitangaza mwenyewe ya kuwa maadhimisho ya uhuru wa Tanganyika ya 9 Disemba yasiwe na sherehe na badala yake siku hiyo iadhimishwe kwa kufanya usafi ili kutokomeza magonjwa yanayolitia taifa aibu hususan kipindupindu.
Watanzania wengi kila mji wametii amri kwa furaha na kutoka tangu asubuhi wakifanya usafi. Wengi wameonekana kufurahia uamuzi wa mh JPM wa kutokuwa na sherehe za uhuru na kuifanya serikali kutunza kiasi kikubwa cha fedha ambazo zitatumika kutoa huduma ktk jamii wa watanzania.
Baadhi ya vijana waliokuwa na mh JPM walisikika wakiimba "Rais wa wanyonge" wakati JPM akifanya usafi.
Je, unaionaje kasi ya JPM na serikali yake ya awamu ya tano... je aendelee bila mawaziri?

Comments

Popular posts from this blog

MAKUNDI CHAMPIONS LEAGUE NA SHIRIKISHO AFRIKA

Yanga Sc kundi A Klabu Bingwa Afrika na Simba Sc kundi A Shirikisho Afrika. Hapo chini ndio mpangilio wa makundi na timu zake. Je, nani kati ya timu zetu za bongo atatoboa kwenda robo fainali? Weka maoni yako kwenye komenti tafadhali.

Hawa Ndiyo Real Madrid Waliowafunga Man City Champions League Jana Usiku

Man City wakiwa wanaongo za kwa 2-1 dhidi ya Real Madrid huku zikiwa zimebaki dakika si zaidi  ya tatu walionekana kama ingekuwa ni timu ya tatu ya Uingereza kuifunga Madrid kwenye uwanja wa Bernabeu. Lakini vijana hao wa Mancini badala ya kuinza kampeni yao kwa ushindi walijikuta wakiachwa nyuma na kuwaangalia Madrid wakiibuka na ushindi baada ya Karim Benzema kusawazisha na kisha Cristiano Ronaldo kufunga goli la tatu na la ushindi, goli lililomfanya bosi wao Jose Mourinho kuslide uwanjani akishangilia goli hilo na Ronaldo. This was the real happiness now from Ronaldo BBC football pundit Robbie Savage alikuwa uwanjani huku Bernabeu. (quoting from BBC SPORTS) "Maicon was not at the races at all in the first half at right-back. He was a passenger and it was like City were playing with 10 men. Cristiano Ronaldo kept coming inside him. "In the second-half, Vincent Kompany looked at what was happening and came across to that wing more. Ronaldo did not...