Jana kulipigwa mtanange wa FA CUP katika dimba la Stanford Bridge kati ya Chelsea na Man City.
mchezo ulianza kwa kawaida sana na hata kuwafanya mashabiki kudhani kuwa wasingefurahia kabisa. Lakini mambo yalianza kubadilika baada ya Chelsea kuanza kuongoza baada ya kutupia goli katika kipindi cha kwanza goli ambalo baada ya muda mfupi sana lilisawasishwa na wapinzani wao Man City.
Kipindi cha pili kilianza kwa majanga kuangukia upande wa vijana wa Manuel Pelegrin ambao walikuwa wametembelea darajani hapo. Magoli yalianza kumiminwa ukiachia lile la Costa mengine yalifungwa na Willian, Hazard, Traore na Cahil.
Wengi wanajiuliza swali hili...
"Kipigo hicho toka kwa Chelsea ni kufuatia ujio wa Pep msimu unao, kwamba Manuel anafanya makusudi? kwani kikosi alichopanga kilijaa makinda wengi sana na hata golikipa alionekana kukosa uzoefu kabisa.. Je, Manuel kajiondoa makusudi ili afokasi kwenye ligi na champions?
Comments